Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa Wanachama wa IAEA wapitisha mpango wa usalama wa nyuklia licha ya kutofautiana

Mataifa Wanachama wa IAEA wapitisha mpango wa usalama wa nyuklia licha ya kutofautiana

Hatua kubwa zimepigwa katika imarisha usalama wa nyuklia duniani tangu ajali ya Fukushima Daichi Japan limesema shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

IAEA imefanya tathimini ya ripoti iliyotayarishwa kwa ajili ya mktano wa kila mwaka wa wanachama utakaofanyika mwezi ujao ambao ulipitisha mpango huo kwa pamoja mwezi Septemba mwaka jana licha ya kukukosolewa kwamba haujitoshelezi.

Shirika hilo linasema baadhi ya maeneo ambayo yamepiga hatua ni pamoja na kuimarika kwa maandalizi na uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura. Fukushima Daichi ilikumbwa na tetemeko na tsunami ambayo ilisababisha kukatika kwa umeme na kuzimika kwa mtambo. Pia watu takribani 150,000 walilazimika kukimbia nyumba zao kutokana na mionzi ya nyuklia iliyokwa ikisambaa hewani.