Watu milioni 2.5 wanahitaji msaada wa haraka Syria:Valerie Amos

16 Agosti 2012

Mratibu Mkuu wa Maswala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura katika Umoja wa Mataifa, Bi Valerie Amos, amesema amekuwa nchini Syria tangu Jumanne ili kujionea mwenyewe athari za mgogoro unaozidi kutokota , na kujadili njia za kuongeza utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Amesema ghasia zimeongezeka, na mara nyingi ukatili unakuwa ni wa kijumla. Amezitaka pande zote husika katika mgogoro wa Syria kujitahidi zaidi kuwalinda raia.

Ameongeza kuwa hali ya kibinadamu imezorota zaidi tangu alipokuwa nchini humo mwezi Machi.

(SAUTI YA VALERIE AMOS)

Ameongeza kuwa watu milioni 2.5 wanakabiliwa na hali mbaya wakati mapigano yanazidi kushika kasi katika maeneo ya raia. Bi Amos ametoa wito kwa serikali na wahisani kuwezesha misaada zaidi kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s kuingia nchini humo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud