Mkuu wa UNDP ahimiza Kuwekeza zaidi katika Kupunguza Hatari za Majanga

15 Agosti 2012

Mataifa ni lazima yawekeze katika kujiandaa na kuzuia majanga, na mataifa yanayotoa misaada na mashirika ya maendeleo hayana budi kuchangia hilo kama suala la kipaumbele katika kuzisaidia nchi maskini, ili maendeleo ya kibinadamu na ya kiuchumi yafanywe badala ya kupotezwa, amesema Bi Helen Clark, Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, ambaye sasa ni Mkuu wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP

Bi Clark ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye chuo kikuu cha Canterbury, nchini New Zealand. Ametumia fursa hiyo kuangazia athari za majanga ya kiasilia dhidi ya watu maskini zaidi, akisisitiza kuhitajika kwa dharura njia za kuzuia na kuziwezesha jamii za watu maskini kujikwamua kutoka taabani kila yanapotokea majanga.

Amesema kwa kila dola moja inayowekezwa katika kupunguza hali ya hatari, takriban dola saba zitaokolewa kutokana na hasara za kiuchumi zinazosababishwa na majanga. Amesema mtazamo wake kuhusu majanga ni kuwa kuzuia ni bora kuliko kutibu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter