Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakaribisha uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu ya Australia

WHO yakaribisha uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu ya Australia

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekaribisha kwa mikono yote uamuzi ulofanywa na Mahakama Kuu ya Australia wa kutupilia mbali kesi ilowasilishwa na sekta ya tumbaku, na kutoa wito kwa mataifa mengine duniani kuiga mtindo wa Australia unaoweka masharti makali kuhusu uuzaji wa bidhaa za tumbaku.

Makampuni kadhaa makuu ya tumbaku yaliipeleka serikali ya Australia kortini, kupinga sheria inayohitaji kwamba sigara na bidhaa nyingine za tumbaku ni lazima ziuzwe kwenye pakiti kavu, bila maandishi yoyote ya kuainisha ya kuwavutia wanunuzi.

Lakini jitihada za makampuni hayo kulegeza njia hii muafaka ya kudhibiti matumizi ya tumbaku, zimeshindwa. Ifikapo Disemba mwaka huu, Australia litakuwa taifa la kwanza kuuza sigara kwenye pakiti zenye rangi isiyopendeza ya mizeituni, bila maandishi ya kuvutia. Glenn Thomas ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA GLENN THOMAS)