Huu ndio wakati ya kumaliza ghasia nchini Syria:Ban

15 Agosti 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema kuwa kilicho muhimu ni kuwa ni lazima vikosi vya serikali ya Syria na vile vya upinzani kusitisha ghasia.

Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari hii leo nchini Timor-Leste Ban amesema kuwa ni lazima wote wasitishe ghasia na kuanzisha mazungumzmo ya kutafuta suluhu.

Ban ameongeza kuwa zaidi ya watu 18,000 wameuawa kwa muda wa miezi 18 iliyopita huku watu wa Syria wakipitia mateso makubwa. Amesema kuwa jamii ya kimataifa ni lazima iungane kukabiliana na hali hii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud