Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lashutumu mashambulizi kwa kikosi cha UNAMID

Baraza la Usalama la UM lashutumu mashambulizi kwa kikosi cha UNAMID

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameshutumu vikali mashambulizi yaliyoendeshwa kwa kituo cha polisi cha kikosi cha pamoja cha Mungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID kwenye mji wa Nyala ulio Darfur Kusini nchini Sudan ambapo mlinda amani mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa.

Wanachama hao wametuma rambi rambi zao kwa familia ya mlinda amani aliyeuwa na kwa serikali ya Bangladesh. Pia wametoa wito kwa serikali ya Sudan kufanya uchunguzi kwa tukio hilo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.