Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu waliotawanywa na Machafuko Syria wanahitaji haraka msaada:Amos

Watu waliotawanywa na Machafuko Syria wanahitaji haraka msaada:Amos

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Valarie Amos ameelezea hofu yake baada ya kukutana na watu waliotawanywa na machafuko wilaya ya Zaheria Damascus katika mwanzo wa ziara yake ya siku tatu Syria na Lebano.

Bi Amos amesema watu aliokutana nao waemwambia wanahitaji maji safi, vifaa vya usafi, madawa na chakula, wanaogopa na wengi hawana nyumba za kurejea hivyo wanahitaji msaada zaidi wa makazi pia.

Katika ziara hii Amos anatumai kujionea mwenyewe athari za machafuko ya Syria na kujadili njia za kuongeza misaada ya kibinadamu.

Amos amekutana na waziri mkuu wa Syria Wael Nadel al-Halqi na kujadili naye umuhimu wa kuruhusu wafanyakazi wa misaada kuingia maeneo yaliyoathirika.

Serikali ya Syria inakadiria kwamba watu milioni 1.2 wamelazimika kukimbia makwao na kuishi kwenye makazi ya muda au kwa familia zinazokubali kuwahifadhi.