IOM yasaidia Waathiriwa wa Usafirishaji Haramu wa watu kutoka Kenya kurudi makwao kutoka Sudan Sudan kusini

14 Agosti 2012

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa wamewasaidia waathiriwa wawili wa usafirishaji haramu wa watu kutoka Kenya kurejea makwao kutoka Sudan kusini. Inaripotiwa kuwa waathiriwa hao ambao ni vijana walitolewa kwenye jamii moja kijijini kwa kazi za nyumbani lakini baadala yake walilazimishwa na kuingizwa kwenye ndoa za lazima.

Walifanikiwa kutoroka ndipo wakapelekwa kwa mashirika ya IOM na UNICEF. Usafirishaji haramu wa watu umetambuliwa kama tatizo linalozidi kushika kasi nchini Sudan kusini huku wale wanaosafirishwa wakipelekwa kufanya kazi za lazima na ukahaba.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud