Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakfu Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, UNRWA wakusanya nguvu kuwalisha Wapalestina 28,000

Wakfu Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, UNRWA wakusanya nguvu kuwalisha Wapalestina 28,000

Wakfu wa Khalifa Bin Zayed Al Nahyan ukishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakipimbizi wa Kipalestina UNRWA umefaulu kuanzisha mpango unaoitwa “ walishe wafungao” kwa ajili ya kuwakirimu wananchi wa Ukingo wa Gaza walioko kwenye kipindi cha mwezi wa Ramadhani.

Chini ya mpango huo kiasi cha watu zaidi 28,000 wanatazamia kufaidika wakipatia misaada ya chakula ikiwemo kupatiwa futari ambayo huliwa wakati wa jioni.

Watu wengi katika eneo hilo wanapata shida ya kupata chakula katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani kutokana na kupanda kwa bei kwa baadhi ya vyakula na hali ya ukosefu wa ajira inayowaandama walio wengi