Mahiga ashutumu vikali mauaji ya afisa wa serikali na mwandishi wa habari nchini Somalia

13 Agosti 2012

Mjumbe maaalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ameshutumu vikali mauaji ya Yusuf Ali Osman ambaye ni afisa wa serikali nchini Somalia na yale ya mwandishi wa habari. Ali au kwa jina lingine Buniste yaliyotokea mjini Mogadishu. Yusuf mwandishi wa habari wa zamani alikuwa mfanyikazi kwenye wizara ya habari na pia ashahudumu kama mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Radio Mogadishu.

Mahiga ametuma rambi rambi zake kwa familia zao na kwa waandishi wote wa nchini Somalia ambao kwa muda mrefu wameshuhudiwa kulengwa , kujeruhiwa na kuuawa kwa wenzao bila ya hata mhusika moja kufikishwa mahakamani. Umoja wa mataifa umekuwa mara kwa mara ukitaka kufanyika kwa uchunguzi ulio huru kwa vitendo kama hivi ambavyo vimeifanya Somalia kuwa moja ya maeneo hatari zaidi duniani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter