Ban Ahusunishwa na Kuangamia kwa watu Kutokana na Tetemeko la Ardhi nchini Iran

13 Agosti 2012

Katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea kaskazini magharibi mwa Iran mwishoni mwa wiki.

Kupitia kwa msemaji wake Ban ametoa rambi rambi zake kwa serikali ya Iran, watu wake na hasa kwa familia za wale waliouawa au kuathiriwa na janga hilo. Kulingana na vyombo vya habari tetemeko hilo lenye uzito kwa 6.4 kwenye vipimo vya richa lilitokea enpeo la kaskazini lililo umbali wa kilomita 60 kutoka mji wa Tabriz na baadaye kufuatiwa na tetemeko lingine dakika 11 baadaye eneo la Varzaghan kilomita 49 kutoka mji huo.

Tetemeko hilo la ardhi lilisababisha vifo vya watu 250 na kuwajeruhi wengine 2,000 na uharibifu kwenye zaidi ya vijiji 11. Utoaji wa misaada unaendelea hata kama ripoti zinasema kuwa shughuli hizo zinatatizwa na mitetemeko mingine midogo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud