Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Azindua Mkakati mpya wa Kulinda Bahari

Ban Azindua Mkakati mpya wa Kulinda Bahari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amezindua mkakati mpya wa kulinda bahari na watu ambao riziki zao zinategemea bahari, na kutoa mwito kwa mataifa kufanya kazi pamoja ili kufikia udhibiti endelevu wa mali ghafi hiyo azizi, na kukabiliana na hatari zinazoikabili.

Kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 30 tangu kufunguliwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria kuhusu bahari, Bwana Ban amesema bahari ni makao ya baadhi ya viumbe wanyonge na muhimu zaidi duniani, ingawa uhai wa viumbe hawa unakabiliwa na hatari inayozidi kuongezeka.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Na taarifa zaidi kuhusu mkakati huo wa kulinda bahari anayo Jason nyakundi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)