Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasaidia juhudi za Ufilipino kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

WFP yasaidia juhudi za Ufilipino kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko

Kufuatia mvua nzito iliosababisha mafuriko katika majimbo ya Luzon ya Kati na Manila Mjini, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa limeandaa misaada ya chakula ili kuisaidia serikali ya Ufilipino katika juhudi zake za kuwasaidia watu waloathiriwa na mafuriko, likisaidiana na idara ya Maslahi ya Kijamii na Maendeleo katika majimbo ya Luzon Kati, Manila Mjini na mengine jirani.

Mkurugenzi Mkuu wa WFP nchini Ufilipino, Stephen Anderson, amesema kuwa amefadhaishwa na athari za kibinadamu za gharika la mvua nchini humo katika kipindi cha wiki moja ilopita, na kuelezea kujitolea kwa shirika hilo kushirikiana na serikali wakati wa dharura. Amesema shirika hilo liko tayari kutoa msaada wake kuimarisha juhudi za serikali kila unapohitajika. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)