Vijana kwenye mstari wa mbele wa kutaka watambuliwe kama watu wenye manufaa kwenye jamii

10 Agosti 2012

Huku mamilioni ya vijana wakiwa hawana ajira kote duniani baadhi yao wameamua kwamba ni vyema wajitokeze, wajionyesha na kujitambusha kwenye sekta mbali mbali duniani angalau kutambuliwa kama walio wenye manufaa makubwa kwa jamii. Baada ya kutambua kuwa hawashirikishwi vilivyo kwenye masuala yanayowahusu baadhi yao wamebuni mashirika yanayowaleta pamoja hasa wanafunzi wanaosomea taaluma mbali mbali na kusafiri nchi tofauti kuonyesha uwezo walio nao na vipawa vyao na kutaka wapewa nafasi ya kuvitumia hasa katika kutimizwa kwa malengo ya Milenia.

Mwandishi wa Nairobi Jason Nyakundi amepata fursa ya kuzungumza na Joseph Muya mmoja wa vijana kwenye kundi la vijana lijulikanalo kama YALDA lililotembea makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya ambaye alikuwa na haya ya kusema.

(MAHOJIANO NA JOSEPH MUYA)