Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi Majirani wa Syria Waendelea Kuwapokea Wakimbizi zaidi

Nchi Majirani wa Syria Waendelea Kuwapokea Wakimbizi zaidi

Ofisi za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Lebanon, Uturuki , Jordan na Iraq zinaripoti kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi kutoka Syria juma hili. Kulingana na takwimu za UNHCR ambazo huonyesha wakimbizi waliojiandikisha na wale walio kwenye shughuli ya kujiandikisha zinaonyesha jumla ya wakimbizi 146,667 hadi Agosti tisa.

Nchini Uturuki idadi ya wakimbizi sasa imepita 50,000 baada ya zaidi ya wakimbizi 6000 kuwasili juma hili pekee wengi wakiwa ni kutoka Aleppo na maneo yaliyo karibu na wengine kutoka Idlib na Latakia. Nchini Iraq kwa sasa kuna wakimbizi 13,587 huku wengi wa wale waliowasili juma lililopita wakiwa kwenye eneo la Kurdistan. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)