Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lapongeza Mpango wa Amani nchini Somalia

Baraza la Usalama la UM lapongeza Mpango wa Amani nchini Somalia

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha hatua zilizopigwa katika kukamilisha majukumu kwenye barabara ya amani ya kumaliza kipindi cha mpito nchini Somalia. Wanachama hao pia wamekaribisha bunge kupitishwa kwa katiba mpya na bunge wakiongeza kuwa kupitishwa kwa katiba hiyo ni hatua muhimu ya mabadiliko nchini Somalia kuelekea kwenye uongozi ulio dhabiti.

Wametoa wito kwa pande husika kuhakikisha kuchaguliwa kwa wanachama wa bunge jipya kunafanyika haraka iwezekanavyo na kwa njia yenye uwazi. Wanachama hao wamelaani majaribio hasa kutoka kwa kundi la wanamgambo la Al-Shabaab ya kutaka kuvuruga mpango huo. Aidha wamepongeza kikosi cha muungano wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia AMISOM na vikosi vya Somalia kwa jitihada zao za kuhakikisha kuwepo usalama wa kutosha kwa pande zote kwenye mpango wa barabara ya amani.