Changamoto za jamii za Watu wa Asili kutoka Bujumbura nchini Burundi

10 Agosti 2012

Kongamano la watu asili kutoka Bara la Afrika limefanyika nchini Burundi wakati UM ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wa asili ambayo inafanyika kila mwaka Agosti 9. Komgamano hilo limeangazia jinsi watu wa Jamii hiyo wanaweza kunufaika na ujuzi wao kupitia haki miliki pamoja na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo wanakoishi.

Watu hao wa asili wamepaaza sauti kwamba haki yao inadhulumiwa na watu ambao wanatumia ujuzi wao wa kiasili kunufaika. Lakini pia Jamii hiyo imekuwa ikinyoshewa kidole kwa kuhusika sehemu kubwa katika uharibifu wa mazingira, madai ambayo wanayakana wakitaja kwamba mazingira ni sehemu ya maisha yao.

Changamoto hizo ndizo zilikuwa mezani katika kongamano hilo la Bujumbura lililonuwia kuweka mtazamo wa pamoja wa watu asili wa bara Afrika, ambao utawasilishwa katika Kongamano Kuu la watu wa asili duniani, baadaye mwezi septemba nchini India.

Kutoka Bujumbura , Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala hii. Ungana nae.

(PKG YA RAMADHAN KIBUGA)