Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakatibisha Muafaka wa pande tatu nchini Sudan

UM wakatibisha Muafaka wa pande tatu nchini Sudan

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Mark Cutts amekaribisha utiaji saini wa maelewano baina ya serikali ya Sudan, kundi la SPLM-North pamoja na Muungano wa Afrika, Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kuhusu msaada wa kibinadamu katika majimbo yaliyoathirika na vita ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Bwana Cutts amesema haya ni maendeleo muhimu sana ambayo ni lazima yatoe fursa ya kuokoa maisha ya watu kwa kuruhusu misaada kupelekwa kwa raia walioathirika na vita ambao wengi wao wamekwa hawafikiwi kwa zaidi ya mwaka sasa.

Mratibu huyo ameongeza kwamba kipaumbele hivi sasa ni kuhakikisha ugawaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu kama inavyohitajika kwa kuzingatia muafaka walioelewana.