Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya Bidhaa za Chakula Yapanda kwa asilimia 6:FAO

Bei ya Bidhaa za Chakula Yapanda kwa asilimia 6:FAO

Bei ya bidhaa za chakula ilipanda kwa kiasi cha asilimia 6 mwezi Julai, baada ya miezi mitatu ya kushuka bei hiyo, limesema Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO.

Kipimo wastani cha viwango vya bei za bidhaa za chakula cha FAO, hupima mabadiliko ya kila mwezi katika bei za kapu la bidhaa za chakula. Kwa kujibu wa Shirika la FAO, nafaka na sukari ndizo zilizochangia kupanda huku.

Mwezi Julai, kipimo wastani kilipanda kwa pointi 12 kutoka mwezi Juni na kufikia pointi 213. Hata hivyo, kipimo hicho kilikuwa chini ya kipimo cha juu zaidi mwaka huu cha pointi 238, kilichoshuhudiwa mwezi Februari. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)