Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada Imara wa Kibinadamu wahitajika DRC:Amos

Msaada Imara wa Kibinadamu wahitajika DRC:Amos

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya dharura na misaada ya kibinadamu Valarie Amos amehitimisha ziara yake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi baada ya kuzuru eneo la Kanyaruchinya nje kidogo ya mji wa Goma siku ya Jumatano. Katika eneo hilo watu 30,000 wamepatiwa makao na amesema inasikitisha kuona watu hususani watoto wanaishi katika hali mbaya.

Amesema Umoja wa Mataifa unajitahidi kufanya kila liwezekanalo kusaidia lakini ni changamoto kubwa kwa mfano eneo hilo halina maji na hivyo inabidi maji kusafirishwa kila siku, huku ukosefu wa fedha, usalama na barabara mbovu ni vikwazo vikubwa vya juhudi za kufikisha misaada .

Hata hivyo Bi amos amewapongeza wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa eneo hilo ambao wanajitahidi kwa kila njia kufikisha msaada kwa wanaouhitaji.