Ban awapongeza Watu wa Asili kwa kutumia Vyombo vya Habari vya Asili na vya Kisasa

9 Agosti 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa asili kwa kujitokeza kutumia vyombo vya habari vya asili na vya kisasa katika kuchagiza masuala mbalimbali yanayowahusu.

Katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya watu wa asili Alhamisi Ban amesema kuanzia magazeti, tovuti hadi mitandao ya kijamii watu wa asili wanatoa changamoto ya kuelezea ukikaji wa haki za binadamu kwa jumuiya ya kimataifa na kutaka kuwepo mshikamano.

Ban amesema kuwa watu wa asili kuanzisha mtandao wao wa habari wataweza kutanabaisha mila na desturi zao na kukabiliana na hadithi potofu na ubaguzi. Pia wataijulisha dunia kuhusu vita wanavyoendelea navyo kwa miongo sasa vya kutotendewa haki na hasa katika kulinda utamaduni wao, lugha zao, imani na desturi zao. ….. ni mku wa watu wa asili wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA……)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter