Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe ni lazima ziwe endelevu:FAO na Bioannuai

Lishe ni lazima ziwe endelevu:FAO na Bioannuai

Hatua zinahitajika kuchukuliwa mara moja ili kuwa na lishe endelevu na mazingira ya uzalishaji chakula, ili kuboresha afya ya wanadamu na ulimwengu wanamoishi, limesema Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO na shirika la Biodiversity International katika kitabu kipya.

Licha ya ufanisi mwingi uliofikiwa katika sekta ya kilimo katika miongo mitatu iliyopita, ni dhahiri kuwa mifumo ya chakula na lishe si endelevu, amesema Bi Barbara Burlingame, Afisa Mkuu wa idara ya lishe na ulinzi wa mlaji ya FAO, katika utangulizi wa kitabu hicho kiitwacho Sustainable Diets and Biodiversity.

Bi Burlingame amesema, wakati zaidi ya watu milioni 900 wanakumbwa na tatizo la njaa, wengine zaidi, takriban bilioni 1.5 hivi, wana matatizo ya uzito mkubwa wa mwili au kunenepa kupindukia, na wengine bilioni mbili kukosa lishe muhimu kama vitamini A, madini ya chuma na Iodine. Bi Burlingame ameeleza ni aina gani ya vyakula watu wanastahili kula, ili kuendeleza lishe endelevu na bayoanuai endelevu.

(CLIP YA BARBRA BURLINGAME)