Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Mali ni wenye Kukanganya na Maumbo tofauti:Ban

Mzozo wa Mali ni wenye Kukanganya na Maumbo tofauti:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa mzozo uliopo nchini Mali ni wenye kukanganya kimawazo na una maumbo tofauti.

Katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bwana Ban amesema kuwa tangu ulipoanza mzozo wa Mali, hali imekuwa ikibadilika na kufikia viwango vya kutisha kila uchao, kila wiki. Amesema ili kuutanzua mzozo huo, itabidi jumuiya ya kimataifa ichukuwe hatua za kina na kamilifu badala ya njia isiyo na mwelekeo kamili.

Ametoa wito kwa serikali ya Mali kubuni njia ya kina ya kisiasa, itakayolirejesha taifa hilo kwenye uongozi wa kikatiba na kuweka tena mamlaka ya kitaifa katika eneo la kaskazini mwake.

Amesema njia hiyo ni lazima iwe mwitikio kwa masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, na kuweka mikakati ya mazungumzo ya kisiasa na kulenga kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya makundi yenye mrengo mkali kaskazini mwa Mali.

(SAUTI  YA BAN KI-MOON)