Mjumbe wa Umoja wa Mataifa ataka Waandishi kupewa Usalama nchini Honduras

8 Agosti 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kutoa maoni na kujieleza Frank La Rue ameanza ziara rasmi nchini Honduras ziara ambayo itakamilika tarehe 14 mwezi huu kwa mwaliko wa serikali. Mjumbe huyo atajaribu kubaini jinsi taifa la Honduras limejiandaa kutekeleza haki ya kujieleza na hatua zilizochukuliwa kuifanikisha na pia changamoto inazokumbana nazo.

Wakati wa ziara hiyo mjumbe huyo atatembelea miji ya Tegucigalpa na San Pedro Sula ambapo atakutana na maafisa wa serikali , wabunge na waakilishi kutoka Umoja wa Mataifa. La Rue pia atafanya mazungumzo na serikali kuhakikisha kuwa watu wote hasa waandishi wa habari wana haki ya kutoa maoni na kujieleza bila ya kuhofia usalama wao. Mjumbe huyo pia atafanya mashaurinao na washirikishi kutoka mashirika ya kimataifa , mashirika yasiyokuwa ya serikali , mashirika ya waandishi wa habari na sekta zingine. La Rue atawasilisha mapendekezo yake kwa baraza la haki za binamdamu mwaka 2013.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter