Skip to main content

Uingereza yaipiga jeki IOM kufanikisha makazi ya waathirika wa mafuriko Pakistan

Uingereza yaipiga jeki IOM kufanikisha makazi ya waathirika wa mafuriko Pakistan

Serikali ya Uingereza imetenga kiasi cha paunti milioni 5 ili kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM ambalo linaendesha shughuli za kuwapatia hifadhi pamoja na chakula kwa mamia wa raia wa Pakistani walioathiriwa na mafuriko msimu uliopita.

Pamoja na mambo mengine kiasi hicho cha fedha kinatazamiwa kuwafaidia zaidi ya familia 10,000 ambazo zimekosa makazi rasmi baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko hayo yaliyopita.

Kulingana na taarifa ya IOM,maeneo mengi nchini Pakistan hasa jimbo la Sindh yamekubwa na uharibifu mkubwa kutokana na mafuriko ya mara kwa mara yanayojitokeza huko.

Kwa sasa kumeanzishwa juhudi za kulijenga upya eneo hilo na tayari tathmini ya mwanzo imefanyika kuibaini mahitajio rasmi.