Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuwafikia watu zaidi na msaada wa chakula nchini Myanmar

WFP kuwafikia watu zaidi na msaada wa chakula nchini Myanmar

Shirika la mpango wa Chakula (WFP) kuwa litaendelea kutoa msaada kwa raia wa Myanmar ambao wamelazimika kuhama makwao na wale walopoteza makazi na riziki zao hadi mwezi Septemba, au hata Disemba mwaka huu.

Tangu mwanzoni mwa mzozo wa Rakhine mwezi Juni, shirika la WFP limewafikia watu waloathirika na zaidi ya tani 2,000 za chakula. Zaidi ya watu laki moja walipata msaada wa vyakula mseto mwezi Juni, na zaidi ya watu 70, 000 mwezi Julai.

Kati ya watu 100, 000 walioathirika, wengi wamesharejea makwao, lakini zaidi ya watu 60, 000 bado wapo kwenye kambi 61, kwenye miji ya Sittwe na Maungdaw, kwa mujibu wa takwimu za serikali. Gharama ya kuwasaidia waathirika kwa kipindi cha miezi 6 kati ya Julai na Disemba ni takriban dola milioni 7.2.