Ukiukaji mbaya wa haki za binadamu waripotiwa kuendelea nchini DRC

7 Agosti 2012

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa ukiukaji mbaya wa haki za binadamu umeripotiwa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ukiwemo mauaji ya kijiji kizima na makundi yaliyojihami, ubakaji, utekaji nyara na kuwaingiza watoto kwenye jeshi.

Kote nchini DRC karibu watoto milioni moja wameathiriwa na hali mbaya ya utapiamlo huku taiafa hilo pia likikikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu. Hadi tarehe 23 mwezi Julai Mwaka huu visa 20,007 na vifo 481 vimeripotiwa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu. Takriban watu milioni 2.2 kwa sasa ni wakimbizi wa ndani mashariki mwa DRC. UNICEF kwa sasa inahitaji zaidi ya dola milioni 133 kushughulikia watoto na wanawake walioathiriwa mwaka huu huku milioni 35.2 zikihitajika kwa dharura. Patrick McCormick ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA PATRICK MCCORMICK)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud