Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yaeleza ongezeko la mahitaji ya kibinadamu Syria

Mashirika ya UM yaeleza ongezeko la mahitaji ya kibinadamu Syria

Shirika la afya dunianin WHO linasema linahofia hali ya afya ya raia nchini Syria. Sekta ya afya ya nchi hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawaa na vifaa vya tiba.

Syria imekuwa ikizalisha asilimia 90 ya tembe na madawa mengine lakini hivi sasa uzalishaji huo unatatizwa na masuala ya usalama, upungufu wa mali ghafi, vikwazo na kupanda kwa bei ya mafuta.

Madawa yanayohitajikamharaka ni pamoja na ya kifua kikuu, ugonjwa wa moyo, kisukari na saratani na yale ya matatizo ya figo. WHO inapeka madawa lakini hayatoshelezi kuziba pengo la upugufu uliopo. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA TARIK  JASAREVIC)

Tathimini ya pamoja ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kilimo na chakula FAO imebaini kwamba watu milioni 1.5 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula katika miezi mitatu hadi sita ijayo hususani katika maeneo ambayo yanashuhudia vita na watu kukimbia. Karibu watu milioni moja wanahitaji msaada wa mazao na mifugo kama mbegu, chakula cha wanyama, mafuta na kukarabati pampu za umwagiliaji.