Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO kutembelea Myanmar kuunga mkono mageuzi ya kisiasa yanayotekelezwa sasa

Mkuu wa UNESCO kutembelea Myanmar kuunga mkono mageuzi ya kisiasa yanayotekelezwa sasa

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova anatazamia kuanza ziara ya siku nne nchini Myanmar ambako pamoja na mambo mengine lakini anatazamia kuweka zingatio lake katika eneo la mageuzi ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.

Katika ziara yake hiyo inayoanza August 7 hadi 10 Bi Bokova anatazamia kuelezea uungwaji wake mkono kuhusu utekelezaji wa mageuzi ya kisasa yanavyochukua mkondo wake mpana.

Atatumia fursa hiyo kujadilia masuala mbambali pamoja na kuwa na majadiliano na maafisa wa serikali kuwaelezea hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa ili kuyalinda mafanikio yaliyoanza kupatikana.

Akiwa nchini humo anatazamiwa kukutana na rais Thein Sein, mwenyekiti wa chama cha kitaifa cha demokrasia ambaye pia ni mbunge Aung San Suu Kyi, na maafisa wengine wa serikali.