Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la haki za msingi za binadamu bado ni changamoto kubwa kwa Myanmar, Mtaalamu wa UM

Suala la haki za msingi za binadamu bado ni changamoto kubwa kwa Myanmar, Mtaalamu wa UM

Juhudi zinapaswa kuchukuliwa sasa kwa taifa la Mynmar kuzitafutia majawabu changamoto zinazojitokeza kwenye maeneo ya haki za binadamu hasa katika wakati huu kunakoshuhudiwa kipindi cha mpiti kuelekea kwenye ujenzi imara wa mifumo ya kidemokrasia.

Kwa mujibu wa mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki za binadamu nchini humo Tomas Ojea Quintana amesema kuwa ili kufanikisha sura ya maridhiano lazima taifa hilo litatua kero zinazojitokeza kwenye maeneo ya haki za binadamu.

Akizungumza wakati akihitimisha ziara yake ya siku sita nchini humo,mtaalamu huyo ametambua hatua kubwa zinazoendelea kupigwa na taifa hilo ikiwemo pia ushiriki mkubwa wa taasisi za kiraia na kutolewa fursa kwa vyama vya kisiasa.

Lakini hata hivyo ametaka kutatuliwa kwa haraka kwa mikwamo ya hapa na pale inayoendelea kukazwa misingi imara ya kuwepo kwa haki za binadamu.