Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa ajili ya Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa ajili ya Syria

Jumuiya ya Kimataifa imetolewa wito na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban kuchukua hatua za kumaliza mgogoro unaoendelea katika Syria.

Bwana Ban amesema haya katika mkutano wa Baraza Kuu wa kupitisha azimio la kulaani vurugu inayoendelea nchini.

Alisema mgogoro wa Syria ni mtihani wa kuwepo kwa Umoja wa Mataifa na kazi yake yote.

"Shinikizo la pamoja la kimataifa l inaweza kuleta mabadiliko. Watu wa syria wanahitaji hatua zichukuliwe. Wamenyimwa matarajio yao. Mateso yao ni makubwa, na ongezeko la hatua za kijeshi itafanya hali iwe mbaya zaidi. Ni wajibu wa wale walio nchini hasa serikali kumaliza mgogoro huu. Hata hivyo kushindwa kwao kuweka slaha chini hakumaanishi sisi wengine hatuna wajibu wa kuchukua hatua. "

Baraza Kuu ilikutana siku moja baada ya Kofi Annan kujiuzulu kama mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria.

Baraza la Usalama limeshindwa kuchukua hatua kuhusu suala la Syria kutokana na kura za Uchina na Urussi za kupinga azimio zilizoletwa mbele ya Baraza hilo.