Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yatoa fedha zaidi kwenye mchango wa kusaidia wakimbizi wa kipalestina

Ujerumani yatoa fedha zaidi kwenye mchango wa kusaidia wakimbizi wa kipalestina

Serikali ya Ujerumani umetoa msaada ya Euro milioni mbili zitakazosaidia kulisha wakimbizi wa kipalestina 667,500 kwenye ukanda wa Gaza. Fedha hizo ni msaada wa ombi la mwaka 2012 la shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbzii wa kipalestina UNRWA la mwaka 2012 la kusaidia wakimbizi kwenye ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi. Mkuu wa UNRWA Filippo Grandi amesema kuwa maelfu ya wakimbizi wa kipalestina wanaokabiliwa na uhaba wa chakula watanufaika kutokana na mchango huu . Hadi sasa Ujerumani imechangia Euro milioni 5.5 tangu shirika la UNRWA litangaze ombi lake.