Mswaaada wa Sharia wafika kwenye bunge la Liberia

3 Agosti 2012

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inahofia mswaada wa sharia ambao hivi sasa umefikishwa mbele ya bunge la Liberia ambo unapendekeza mabadilikon ya sheria ambayo yatafanya kuwa ni uhalifu tabia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Sheria ambayo imeshapitishwa na bunge l seneti infany kuwa ni kosa la jinai la kiwango cha pili ikimaanisha kwamba adhabu yake ni kifungo cha miska mitno jela au zaidi nap engine faini kwa mtu atakayechagiza, kushawishi au kuwataka watu wengine wa jinsia moja kushiriki ngono.

Ofisi ya haki za binadamu pia inatiwa mashaka na mazingira ya kuwatisha na kufanya ghasia dhidi ya wanawake na wanaume wanaoshiriki ngono ya jinsia moja na pia taarifa za mashambulizi dhidi yao. Ofisi inasemsa vitendo hivyo vinaashiria ugumu, na mazingira ya ubaguzi ambayo wanaishi wapenzi wa jinsia moja na kwamba sheria ikipitishwa na bunge itafanya hali ambayo tayari ni mbaya kwa wapenzi wa jinsia moja Liberia kuwa mbaya zaidi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter