Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Google and ITU washirikiana kutoa bure kimataifa takwimu za teknolojia

Google and ITU washirikiana kutoa bure kimataifa takwimu za teknolojia

Takwimu za muungano wa kimataifa wa teknolojia ya mawasiliano ITU na teknolojia ya mawasiliano ICT sasa zinapatikana kupitia mtandao wa umma wa utafutaji takwimu yaani Google Public data Explorer kupitia kwenye wavuti.

Kwa ushirikiano wa mtandao wa Google na ITU sasa watumiaji wa mtandao wanaweza kutafuta na kuona takwimu muhimu zilizopo za teknolojia ya mawasiliano kuanzia mwaka 1960 hadi 2011 za nchi karibu 200 duniani.

Viashiria muhimu vya takwimu hizo ni pamoja na simu za ndani, internet, simu za mkononi, matumizi ya broadband na asilimia ya watu binafsi wanaotumia internet. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)