Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na Mashirika yasiyokuwa ya serikali watoa huduma kwenye kambi ya Yida

UNHCR na Mashirika yasiyokuwa ya serikali watoa huduma kwenye kambi ya Yida

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wanafanya juhudi kukabilina na visa vya utapiamlo, magonjwa na vifo kwenye kambi mbili zinazowahifadhi wakimbizi kutoka Sudan.

Wahudumu wa afya kwenye kambi ya Yida jimbo la Unity walishuhudia kuongeza kwa vifo kwa watoto kwemye kambi mwezi Juni na mapema mwezi Julai. Mwa muda wa majuma matatu yaliyopita vifo vimeripotiwa kupungua baada ya mashirika ya kutoa misaada kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

UNHCR na mashirika mengine yasiyokuwa serikali wamekuwa wakitoa huduma ya siku 40 kusafirisha vituo vya maji. Kambi ya Yida kwa sasa inawahifadhi wakimbizi 60,000 kutoka jimbo la Kordofan kusini nchini Sudan Kusini huku watoto wakichukua karibu robo ya idadi hii. Melissa Flemming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMMING)