Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafungua Ofisi Dollo wakati Wasomali wakizidi kukimbia Ukame

UNHCR yafungua Ofisi Dollo wakati Wasomali wakizidi kukimbia Ukame

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefungua ofisi mjini Dollow na kurejesha uwepo wake kwenye mji huo wa karibu na mpaka wa Somalia na Ethiopia ili kukabiliana na ongezeko la wakimbizi wa Somalia wanaokimbia ukame.

Takwimu za karibuni zinaonyesha kwamba watu 11,000 zaidi wametawanywa ndani ya Somalia tangu mwanzo wa Aprili kutokana na ukame na maisha duni na hao ni zaidi ya wale 7000 waliotawanywa katika robo ya kwanza ya mwaka huu kwa sababu hizohizo.

Kufunguliwa kwa ofisi hiyo Dollow ambako ni makazi ya wakimbizi wa ndani wa Somalia 7600 na kilometa chache kutoka makamb ya wakimbi ya Ethiopia ya Dollo Ado kutaruhusu UNHCR kwa karibu wakimbii wanaoingia mipakani.

Pia kutaisaidia UNHCR kuingia ndani ya Somalia kufikisha msaada kwa maeneo yanayofikika. Ofisi hiyo itatumika pia na mshirika mengine sita ya Umoja wa Mataifa na itakuwa ni kituo cha opertesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa.