Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasema linatupia macho hali za kibidamu nchini Syria

Baraza la Usalama lasema linatupia macho hali za kibidamu nchini Syria

Huku machafuko yakizidi kuchacha nchini Syria mnamo wakati mjumbe maalumu wa upatanishi kwenye mzozo huo Kofi Annan akiashiria kuachia wadhifa wa usuluhishi ifikapo mwishoni mwa mwezi huu,Baraza la Usalama linatafakari hatma ya raia milioni 3 walioko kwenye hali mbaya wakihitaji msaada wa dharura.

Wakati huu Ufaransa imechukua kiti cha urais wa kupokezena katika baraza hilo la usalama na imesema kuwa kuna mataifa yameanza kukata tamaa kuhusiana na hali jumla ya mambo nchini humo.

Ufaransa imesema kuwa bado jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa zingatio la kutosha kwenye eneo hilo na kuna utashi wa kutosha kutambua shida na mateso yanayowaandama mamilioni ya raia ambao wapo kwenye mkwamo wa huduma za kibinadamu.