Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka Waasi wa M23 kuacha Mapigano

Baraza la Usalama lataka Waasi wa M23 kuacha Mapigano

Baraza la Usalama limerejelea mwito wake kutaka makundi ya askari waasi wanaoendesha vitendo viovu huko kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuweka silaha nchini kwa mustakabala wa taifa hilo na wananchi wake.

Baraza hilo limesema kuwa kundi la askari waasi wa M23 wanapaswa kujieopusha na matumizi ya silaha kuzorotesha usalama katika eneo walikopiga ng’ome huku wakitakuwa pia kutotoa vitoshi vya kutaka kuteka maeneo mengine zaidi.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari,baraza hilo lenye wajumbe 15 limelaani vikali matukio ya mashambulizi yanayoendeshwa na vikosi hivyo na kusisitiza kuwa vinapaswa kuweka silaha nchini mara moja na kujiepusha na vitendo vyovyote vya uhalifu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia..