Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imefanya Ushirikiano na Wizara ya afya nchini Uganda kudhibiti ugonjwa wa Ebola

WHO imefanya Ushirikiano na Wizara ya afya nchini Uganda kudhibiti ugonjwa wa Ebola

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa kwa sasa kumeripitiwa visa 50 vya ugonjwa wa Ebola na vifo 16 vilivyosababishwa na ugonjwa huo nchini Uganda. Tangu siku ya Jumanne visa kadha vya ugonjwa huo vimeripotiwa hospitalini lakini ni watu wawili walioripotiwa kuaga dunia.

Wizara ya afya nchini Uganda inashirikiana na washikadau pamoja na washirika wake kuudhibiti ugonjwa huo ambao umeripotiwa sehemu za magharibi mwa nchi. WHO kwa upande wake imetuma wataalamu na vifaa 800 vya kujikinga vitakavyotumiwa na wahudumu wa afya na wale wanaokaribiana na watu walioambukizwa. Nalo shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda linafanya juhudi za kuwahamasisha watu kuhusu ugonjwa wa Ebola.