Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yajenga Vituo vya Afya Kuwasaidia jamii ya waliokosa makazi Zimbabwe

IOM yajenga Vituo vya Afya Kuwasaidia jamii ya waliokosa makazi Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM leo limekabidhi vifaa tiba kwa vituo vya afya vinavyotoa huduma za utabibu katika maeneo ya vijijini vilivyoko kusini mashariki mwa mji wa Harare.

Vifaa hivyo lakini vinatazamiwa kuwa habari njema kwa mamia ya waliokuwa wafanyakazi wa mashambani ambao wengi wao hawana makazi maalumu

Kiasi cha wafanyakazi wa mashambani 160,000 walipoteza kazi zao na hivyo kusalia kuishi maisha ya kubangaiza na wengi wao wakikosa makazi rasmi wakati serikali ya Zimbabwe ilipoanzisha sera ya ardhi ya mwaka 2000

Vituo hivyo vya afya vinavyopatikana katika maeneo ya Zunidza na Makoni vinatazamia kuwafaidisha zaidi ya wakazi 3500 waliotambuliwa kama zingatio la kwanza