Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHC yasema kuwa vikosi vya usalama vimewaua watu wakati maaandamno kwenye jimbo la Darfur

OHCHC yasema kuwa vikosi vya usalama vimewaua watu wakati maaandamno kwenye jimbo la Darfur

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema kuwa vikosi vya usalama kwenye jimbo la Darfur huenda viliwaua watu wannane ambapo watano kati yao walikuwa ni wanafunzi walio na umri wa chini ya miaka mitano na kuwajeruhi watu wengine 50 siku ya Jumanne wakati walipowafyatuilia risasi waandamanaji kwenye mji wa mji mkuu wa jimbo la Darfur kusini Nyala.

Walioshuhudia wanasema kuwa kulitumika gesi za kutoa machozi na risasi. OHCHR imeishauri serikali kuaazisha uchunguzi huru hasa kilichopelekea matumizi ya nguvu kupita kiasi na vikosi vya usalama. OHCHR inasema kuna mipangilio ya kimataifa inayostahili kufuatwa wakati wa maandamano kuhakikisha haki za watu za kujieleza na kukusanyika zimeheshimiwa.

CLIP: (Ravina Shamshadani ni msemaji wa OHCHR )