Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawapa Mafunzo Wafugaji nchini Kenya

IOM yawapa Mafunzo Wafugaji nchini Kenya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha shughuli ya kuwapa mafunzo wafugaji 180 kutoka maeneo sita kwenye wilaya ya Daadab kaskazini mwa Kenya kuhusu jinsi watakavyowatunza mifugo wao wakati kunapotokea ukame.

Ufugaji wa ng’ombe ndio tegemeo kwa wenyeji wa kaskazini na kaskazini masharki mwa Kenya walioko maelfu ya wasomali wanaokimbia vita na ukame nchini mwao. Eneo hilo ndiko kuliko kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani yenye wakimbizi 453,000 kutoka Somalia. Wakati wa kipindi cha ukame maelfu ya mifugo huangamia kutokana na ukosefu wa malisho na magonjwa. Kuwasili kwa wakimbizi kutoka Somalia inakuwa ni changamoto kwa wafugaji changamoto ambayo huleta misukosuko wanapong’angania raslimali chache zilizopo. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)