Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasaidia waathirika wa Mafuriko DPRK

UM wasaidia waathirika wa Mafuriko DPRK

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK wanatoa msaada wa chakula, vifaa visivyo chakula, madawa, maji na vifaa vya usafi kufuatia athari za mafuriko nchini humo.

Mashirika hayo yanatarajiwa kuendelea kusaidia kutokana na mahitaji ya watu wa DPRK. Wakati kipaumbele kimetolewa kwa nchi ambazo zimemetembewa, msaada wa kibinadamu pia utatolewa kwa nchi zingine zilizoathirika na mafuriko hayo.

Tathimi ijayo ya mazao na usalama wa chakula itakayofanyika mwei Septemba na Oktoba mwaka huu itatathimini athari za mafuriko hayo katika uzalishaji wa chakula.