Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bima inaweza kusaidia kuwalinda maskini dhidi ya Ongezeko la joto duniani:ILO

Bima inaweza kusaidia kuwalinda maskini dhidi ya Ongezeko la joto duniani:ILO

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO hali ya hewa haiwezi kuwekewa bima lakini baadhi ya athari zake zinaweza kukatiwa bima hata kwa masikini ambao huathirika zaidi na athari za ongezeko la joto duniani. Craig Churchill ambaye anaongoza kitengo cha ILO kinachohusika na masuala ya bima anasema licha ya changamoto, kwa msaada wa ruzuku, tekinolojia, mitazamo ya ubunifu na mifumo ya bima vinaweza kuwa nguzo muhimu katika kupunguza athari za majanga ya hali ya hewa na ongezeko la joto kwa masikini.

Kwa mujibu wa ripoti ya ILO kitengo cha bima ya majanga cha Caribbean CCRIF, ni moja ya vitengo ambavyo vinasaidia sana kwani kinatoa bima ya gharama nafuu kuliko ile ya serikali katika maeneo ambayo yameathirika na vimbunga na hivyo kutoa matumaini kwa watu wengi wasiomudu bima za gharama kubwa.