Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka Amani idumu wakati wa Kuhamishwa kwa Watoro wa Iran kutoka kambi nchini Iraq

Ban ataka Amani idumu wakati wa Kuhamishwa kwa Watoro wa Iran kutoka kambi nchini Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amezitaka pande mbili husika kushirikiana na kukamilisha kwa amani kuhamishwa kwa watoro wa Iran waliosalia kwenye kambi moja nchini Iraq. Kuambatana na makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi Disemba kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Iraq ni kwamba theluthi mbili ya watu au 2000 wamehamishwa kwenda kituo kilicho karibu na mji wa Baghdad ambapo mpango wa kuwatambua kama wakimbizi unaendeshwa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Karibu watu 1,300 watoro wa Iran ambao wengi ni wa kundi lijukanalo kama People’s Mojahedeen of Iran bado wanasubiri kuhamishwa kutoka kambi hiyo. Ban ameipongeza serikali ya Iraq kwa moyo wa ushirikiano ambao imeonyesha miezi kadha iliyopita hatua ambao imechangia kuhamishwa kwa watu hao kwa njia ya amani.