Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuendelea kutoa Msaada wa Chakula kwa Wakimbizi wa Sudan Kusini

WFP kuendelea kutoa Msaada wa Chakula kwa Wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema lina mpango wa kuendelea kutoa msaada unaohitajika haraka wa chakula kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi kwenye jimbo la Upper Nile Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WFP Sudan Kusini Chris Nikoi wakimbizi wanaowasili kamimbini huwa wamedhoofu na wenye njaa baada ya kusafiri wiki kadhaa msituni kabla ya kuingia mpakani.

Ameongeza kuwa msaada wa WFP umekwa umeokoa maisha ya wakimbizi zaidi ya 100,000 kwenye kata ya Maban na kuendelea kutoa msaada ho knahitaji hatua madhubti ikizingatiwa idadi ya wakimbizi wanaoingia kila siku ni kbwa na miundombinu ni duni. Katika juhdi hizo za kuokoa maisha WFP inasema ina mipango ya kupeleka tani 2000 za chakula kitakachokuwa kikidondoshwa kwa ndege kwenye eneo la Maban kuanzia katikati ya mwezi huu.