Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WaSyria milioni 3 wanahitaji msaada wa Chakula, Mazao na Mifugo:FAO na WFP

WaSyria milioni 3 wanahitaji msaada wa Chakula, Mazao na Mifugo:FAO na WFP

Takribani watu milioni tatu wanahitaji msaada wa chakula, mazao na mifugo nchini Syria kwa mujibu wa tathimini ya karibuni iliyopfanywa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria.

Watu milioni 1.5 kati ya hao wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita ijayo na hususani kwenye maeneo ambayo yanashuhudia vita na watu kuzikimbia nyumba zao. Watu wengine milioni 1 wanahitaji mazao na mifugo kama mbegu, chakula cha mifugo, mafuta na kukarabati pampu za umwagiliaji. Tathimini hiyo ya pamoja ya mahitaji ya haraka ya usalama wa chakula imefanywa na shirika la chakula na kilimo FAO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na wizara ya kilimo ya Syria. Abeer Etefa ni afisa mawasiliano wa WFP mjini Cairo.

(SAUTI YA ABEER ETEFA)

Ripoti ya mwisho ya tathimini hiyo inasema sekta ya kilimo0 ya Syria imepoteza jumla ya dola bilioni 1.8 mwaka huu kutokama na machafuko yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na hasara na haribifu wa mazao, mifugo na mfumo wa umwagiliaji.