Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu Ban ashtumu Mashambulizi katika mji mkuu wa Somalia

Katibu Mkuu Ban ashtumu Mashambulizi katika mji mkuu wa Somalia

Ugaidi ni lazima usiruhusiwe kurudisha nyuma mafanikio muhimu katika mchakato wa amani unaoendelea wa kuunda serikali mpya na taasisi za kudumu nchini Somalia.

Huu ndio ujumbe wa Katibu Mkuu, katika taarifa aliotoa kufuatia jaribio la kushambulia jengo ambapo Mkutano wa Kimataifa wa Baraza la Katibu uliokuwa ukifanyika, kupitisha katiba mpya leo Jumatano.

Katibu Mkuu amekaribisha kupitishwa  kwa katiba ya muda ya Somalia na kuwapongeza wajumbe na uongozii wa Somalia kwa kile alichokiita “mafanikio ya kihistoria”

Msemaji wa Katibu Mkuu Martin Nesirky anaelezea zaidi.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)