Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya miaka Takribani 40 Somalia yapata Katiba Mpya:Mahiga

Baada ya miaka Takribani 40 Somalia yapata Katiba Mpya:Mahiga

Viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia na wawakilishi wa majimbo yote ya nchi hiyo wanaokutana Moghadishu wamepitisha kwa wingi wa kura katiba mpya  ambayo inafungua mlango wa kuchaguliwa kwa serikali mpya mwezi huu. Jumla ya wawakilishi 825 walikuwa wakijadili kuhusu katiba hiyo kwa juma zima na 621 wamepiga kura ya ndiyo, 13 wamepinga na 11 hawakupiga kura kabisa.Kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo balozi Augstine Mahiga huu ni mwanzo wa ukurasa mpya Somalia, na viongozi wanathibitisha kuheshimu mchakato wa kisiasa nchini humo. Amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kuhusu hatua hiyo muhimu ya leo.

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)