Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua mwanadiplomsia wa Austria kama mratibu wa Masuala ya Wingi wa Lugha

Ban amteua mwanadiplomsia wa Austria kama mratibu wa Masuala ya Wingi wa Lugha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua msaidizi wake wa masuala ya mawasiliano na habari kwa umma Peter Launsky-Tieffenthal kuwa mratibu wa masusla ya wingi wa lugha.

Uteuzi huo unajiri baada ombi la baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa Ban wa kumataka amteue afisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa kuchukua wadhifa huo. Tangu mwaka 2007 bwana Launsky amehudumu kama mkuu wa idara ya mawasiliano nchini Austria na pia ana ujuzi wa miaka 30 akihudumu kwenye wizara ya mambo ya kigeni barani Asia na mashariki ya kati kama mwanadiplomasia.